Social Responsibility

Karibuni

Shahada ya “Social Responsibility,” iliyoanzishwa kwa kushirikisha ahali za kibinadamu, “sociology”, na mafunzo yahusiyo wanawake inazingatia wajibu wa kila raia kwa kila mmoja, jamii na mazingira kwa ujumla. Inatoa mafunzo mahususi kwa nadharia na vitendo kuhusu uwajibikaji kwa kuzingatia historia na herimu. Programu inatoa maarifa kwa vitendo kwa raia washiriki na kuwapa uwezo wa kushiriki kutoa huduma katika maeneo yao, majimbo yao, nchi zao pamoja na dunia nzima kwa ujumla kwa kuzingatia na kuheshimu demokrasia na tamaduni mbalimbali. Mifumo bunifu katika masuala muhimu ya usawa, mgawanyo wa raslimali, kazi, elimu, afya, usalama, na mazingira endelevu yanazumbuliwa katika upeo wa kibinafsi, kitaaluma na kidunia nzima kwa ujumla. Kwa kina, mtaala unatoa elimu na mafunzo katika utaifa, jinsia, matabaka, ulemavu, herimu, uraia, matabaka katika jinsia, viumbe, kazi, haki za binadamu duniani, na mazingira.Wahitimu katika masomo yao watakuza upeo wao katika ustadi katika utafiti wa kina, uchunguzi, mpambanuo, na uandishi katika masuala mbali mbali duniani.

Kwa kuwa masuala muhimu ya matabaka katika jamii na dunia endelevu yanajitokeza na kuwa bayana katika kila jamii nguzo madhubuti katika kila taaluma dadisi zimekuwa zikianzishwa katika nyanja zilizo nyingi za awali na zinazojitokeza ambazo kwa pamoja zinatathmini nadharia, miundo na mifumo ya uwajibikaji katika jamii. Mafunzo ya uwajibikaji katika jamii (“Social Responsibility”), hayakulengwa kukidhi dhana moja iliyokuwapo, bali ni programu yenye kuzingatia na kuunganisha taaluma kadhaa wa kadhaa, ni programu ambayo imehusisha nyanja tofauti tofauti kama vile utu wa binadamu, sayansi ya jamii, taalimu, sayansi na teknolojia. Shahada hii ya uwajibikaji katika jamii inatoa elimu na taaluma kwa washiriki wenye mtizamo wa kushirki katika nyanza hizi. Mafunzo katika programu hii yanakidhi kwa mapana yake katika nyanja mbali mbali kukuza kwa ustadi taaluma kwenye nafasi kadhaa wa kadhaa kwenye taasisi zilizo na zisizo kuwa za kiserikali zinazojihusisha na elimu, mawasilianao, uongozi, afya, mashauri. Pia programu inatoa fursa kwa wahitimu kuwa na uwezo wa kufanya kazi katika ngazi za nchi na kimataifa. Aidha mpangilio wa ratiba katika programu hii inatoa fursa kwa washiriki kuhitimu na kupata shahada wakiwa wanafunzi wa muda wote au kwa kuhudhuria masomo ya jioni.

For questions or more infomation, please contact:
Menan Jangu (jame0201@stcloudstate.edu)

Required Courses | About the Program | Faculty | Graduates
Careers | Honors & Activities | Newsletter | Faculty Articles
Links | Internships | Assistantships | Calendar | Home